M |
Nidhamu ndiyo chanzo cha mafaniko yoyote ambyo mtu anatamani kuyafikia katika kutimiza ndoto zake .Mafanikio ya mtu hupimwa pindi anapokuwa ameanza kuishi ndoto zake ,mafanikio ambayo mtu anatafuta katika maisha ya kila siku yamegawanyika katika makundi makuu matatu
1 Mafanikio kiuchumi.
Hili ni kundi mojawapolakupima mafaniko ya mtu , kwani ni ukweli usiopingika kuwa watu wengi hutamani sana kufanikiwa katika eneo la uchumi , kwa sababu mafanikio ya kiuchumi hufungua milango ya mafanikio mengine .Watu walio fanikiwa kiuchumi ndio pia wana nafasi ya kufikia mafanikio ya makundi mengine kwani mafanikio haya pia huleta pesa za kutosha ambazo ndo hizo zinazo leta jawabu la mambo yote( MUHUBIRI 10:19C)
2 Mafanikio kisiasa
Siasa ndiyo ambayo hutawala sana karibu mifumo yote ya kiutawala ambapo utawala uaotawala eneo flani ndio unao amua ana ya mfumo wa kiuchumi wa eneo hilo .Wanasiasa wengi hutamani sana kufanikiwa katika eneo hili .Jambo moja muhimu ni kujua umuhimu wa kuwa na nidhamu ya kufatilia sana mambo ya husuyo siasa ili kupata taaifa nyingi na maarifa mengi ambayo yatakusaidia katika kufikia mafanikio kwenye eneo hili la siasa
Kama unataka ufanikiwe katika siasa anza leo kuweka nidhamu ya kufatilia sana maswala ya siasa ili kupata taarifa sahihi na maarifa mengi na utaona matokeo yatakayo kufikisha kwenye eneo hili
3 Mafanikio kiroho
Ni wazi kuwa kila mtu kutokana na imani yake katika dini yake anatamani sana kukuwa kiimani (kiroho) na kukuwa huko kiimani(kiroho) hapo tunasema mtu huyu amefanikiwa
Licha ya mafanikio kugawanyika katika makundi makuu matatu nayo hutegemea mambo makuu matatu ambayo ni fedha , mda na mipango mizuri
Leo napenda tuangalie nguvu ya nidhamu katika fedha , mda na mipango mizuri ili kufikia mafanikio hayo
1 Nidhamu ya fedha
Fedha huleta jawabu la mabo yote (MUHUBIRI10:19C) ,ikiwa na maana kuwa fedha ndiyo nguzo ya kwanza katika kuleta mafanikio makubwa kiuchumi , kisiasa na kiroho ikiwa tu utakuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha .Nidhamu nzuri ya fedha husaidia katika kutekekeza mipango mizuri ili kufikia mafanikio . Mafanikio yako hayategemei wingi wala uchache wa fedha ulizo nazo bali hutegemea nidhamu katika matumizi ya kiasi cha fedha katika kuleta mafanikio .
2 Nidhamu katika matumizi ya mda
Waswahili husema mda ni mali lakini kama haujui dhana halisi ya usemi huu utaona kama ni jambo la kawaida sana ,hata mimi kabla sijaelewa dhana ya msemo huu nilijua kuwa kitu cha msingi sana katika maisha ni kuweka nidhamu katika fedha na sio matumizi mazuri ya mda ,lakini baada ya kujua thamani ya mda ningependa nukufahamishe nguvu ya nidhamu katika matumizi ya mda .Mungu ametupa mda wa masaa ishirini na nne (24) kila siku sawa na masaa elfu saba mia nane na sitini(7860) kwa mwaka mzima ila ni mda huohuo wapo watu matajili na watu masikini sana ,hivi umewahi kujiuliza kwa nini watu wengi sio matajili au kwa nini watu wengi hawana mafanikio mkubwa lakini kuna wachache wamefanikiwa sana wakati wote hao wana mda sawa kwa kila siku,siri kubwa ni kwenye nidhamu ya matumizi ya mda .Mafanikio yako yanategemea sana jinsi unavyo tumia mda wako vizuri katika kutimiza malengo yako.
Anza leo kuwa na nidhamu katika matumizi ya mda katika mambo uliyopanga kuyafanya utaona matokeo
3 Nidhamu katika kutekeleza mipango yako
Kupanga ni kuchagua ,usemi huu umezoeleka sana masikioni mwa watu wengi sana ,lakini leo napenda nikwambie nguvu ya nidhamu katika kutekeleza mipango inavyoleta mafanikio haraka,katika mpango wowote katika kuleta mafanikio kuna vitu vinaitwa vipaombele na maana ya vipaombele ni vitu vya msingi katika mpango wowote ambapo mafanikio ya lengo lolote hutegemea kukamilika au utekelezaji mzuri wa hivyo vipaumbele .ni wazi kuwa kila mtu ana mipango mbalimbali ya kutekeleza ili kufika mafanikio anayotaka na katika mipango hiyo kuna mikakati mbalimbali ya kutekeleza ili kufikia malengo hayo ,kitu cha muhimu kujua ili uweze kufanikiwa katika kufikia malengo yako ni kuweka nidhamu katika kutekeleza vipaumbele vitakavyo fanikisha mpango wako ,kwa maneno mingine ni kusema usikubali kutekeleza kipaumbele hata kimoja kwani kushindwa kukamilika kwa kipaumbele kimoja husababisha kushindwa kwa kukamilika mpango mzima ambao ndio ungekupelekea kufikia malengo yako . kinachotofautisha kati ya waliofanikiwa na amabao hawajafanikiwa ni nidhamu katika kutekeleza vipaumbele vya mpango wa kufikia malengo
Anza leo kuhakikisha unaweka nidhamu katika kuteleza vipaombele vya mpango uliojiwekea utaona matokeo mazuri sana katika kufikia malengo yako
Hitimisho
Watu wote duniani walio fikia malengo yao walikuwa na nidhamu katika matumizi ya mda,fedha na mipango hata wewe haujachelewa anza leo kuwa na nidhamu katika matumizi ya mda ,fedha na mipango nakuhakikishia kuwa utafikia malengo yako
No comments:
Post a Comment