JAMBO MOJA MUHIMU LA KUJUA ILIUWEZE KUFANIKIWA HARAKA KATIKA JAMBO ULIFANYALO
Kila binadamu anapenda kufanikiwa haraka juu ya jambo alifanyalo ili kujieletea mafanikio yake binafisi na jamii kwa ujumla .Lakin uli ufanikiwe haraka kuna mabo muhimu ya kujua.Leo ningependa tuangalie jambo moja muhimu la kujua ili uweze kufanikiwa haraka katika jambo ulifanyalo
Jambo la kwanza ni kujua uwezo wako
Ni wazi kuwa binadamu tunatofautiana katika uwezo wa kufanya mambo mbalimbali na ni uwezo huohuo ndio unaotafautisha mafanikio ya mtu moja na mwingine.Katika kutambua uwezo wako kuna mambo matatu muhimu ya kuangalia.
1. Uwezo wa kiakili
Uwezo wa kiakili hutofautiana kati ya mtu moja na mtu mwingine ,uwezo huo umegawanyika katika makundi mawili :
Kundi la kwanza ni uwezo wa kuelewa haraka ,hili ni kundi mbalo watu wa kundi hili wanauwezo wa kuelewa mambo haraka na kufanya wafanikiwe haraka katika mambo wayafanyayo kutona na uwezo huo mambo yao hufanyika haraka sana na kwamafaniko makubwa sana.
Kundi la pili ni uwezo wa kuelewa polepole,kundi hili la uwezo wa kiakili mara nyingi watu wa kwenye kundi hili huelewa mambo taratibu sana lakini mwisho wa siku wanafikiwa katika malengo yao .Hapa ndo utaona wanafunzi wapo wanaosoma kwa mda mrefu sana na wengine mda mfupi sana na wanafanya vizuri sana
Leo ukitambua uwezo wako utakuwa umepata siri kubwa ya kuweza kufanikiwa kwa kila jambo ulifanyalo
2.Uwezo wa kifedha
Fedha huleta jawabu la mambo yote( MUHUBIRI 10:19)
Kila binadamu ili aweze kufanikiwa katika jambo flani huhitji fedha ili kufanikisha ndoto zake .Kwa hiyo jambo lolote la mafanikio linagharama ambayo lazima fedha itumike kwa namna moja na nyingine .kujua uwezo wako wewe wa kifedha kutakusaidia kujua kama utakuwa tayari kuingia gharama hizo, vinginevyo utajikuta unaaanzisha jambo flani na unaishia njiani bila mafanikio
3.Uwezo wa nguvu za mwili
Niukweli kuwa kila jambo alifanyalo mtu huhitaji nguvu ya mwili .Hivyo ili ufanikiwe haraka katika jambo ulifanyalo ni muhimu kujua uwezo wako wa mwili juu ya jambo hilo vinginevyo utajikuta unafanya mambo mkubwa sana ambayo yanhitaji nguvu nyingi na kutokana na kutokuwa na nguvu ya kimwili ya kukuamilisha jambo hilo utashindwa kufanikiwa , kufanya jambo uliwezalo kimwili husaidia kufikia mafanikio haraka sana
Hitimisho
Mafanikio yoyote ya mtu hutegemea sana uwezo wake wa kiakili, kifedha na kimwili .Hivyo umakini katika kujua uwezo wa kiakili , kifedha na kimwili ndio hufanya mtu kuwahi kufanikisha jambo alifanyalo kwa kuwa utafanya jambo au kitu ambacho utakuwa na uwezo nao .Anza leo kutambua uwezo wako katika kila jambo ulifanyalo ili uweze kufanikiwa haraka
Ubarikiwe sana msomaji wangu
kwa maoni na ushauri niandikie kwa barua pepe
novathkasiano@gmail.com au piga simu kwa namba +255 753 485 656
No comments:
Post a Comment