MAMBO 3 YANAYO CHELEWESHA MTU KUFANIKIWA KIUCHUMI
Mpendwa msomaji wangu leo napenda tujifunze juu ya mambo ambayo husababisha mtu kuchelewa kupata mafanikio ya kimaisha .
Kila binadamu aliyeumbwa na Mungu hutamani sana kuwa na mafaniko makubwa sana kiroho na kiuchumi .Katika jitihada za kufikia mafanikio hayo kila mtu huomba Mungu kulingana na imani yake ,lakini pamoja na jitihada hizo za kumuomba Mungu ili kufanikiwa kiuchumi yapo mambo makuu matatu yanayo chelewesha mafanikio yako katika misingi sahihi
(1) KUTOKUJUA KUSUDI ULILOITIWA KUTIMIZA
Ni mpango wa mungu kumuumba mwanadamu ili alitimize kusudi lake ,lakini watu wengi sana wapo hapa duniani na hawajui kusudi lililo waleta kulitimiza hapa duniani hali ambayo inapelekea kuishi nje ya mpango wa mungu na kusababisha kuchelewa au kushindwa kabisa kupata kile wanacho sitahili kupata .Mungu anakujua hata kabla hajakuumba ,ila anachotaka kwako ni wewe kumuuliza Mungu ujue kusudi alilokuitia ili uweze kulitimiza ,mfano Yeremia aliitwa kuwa nabii (Yermia 1:5) ukitambua kusudi la wewe kuwepo hapa duniani itakuwa rahisi kufikia mafanikio yako haraka
(2) KUTOKUSIKIA MAAGIZO YA MUNGU
Ni mpango wa mungu kwa mwanadamu kufanikiwa katika mambo yote ila usipo sikiliza maagizo ambayo mungu anakuagiza kufanya kila siku utachelewa kupata mafanikio kwani kila utakalo lifanya litakuwa nje ya mapango wa mungu .Mungu ame ahidi kukupa mambo mengi sana kama uko tayari kuyasikiliza na kuyafanyia kazi maagizo akuamuruyo kuyafanya kila siku utapata baraka nyingi sana ambazo zitakupeleka katika mafanikio ya kimwili na kiuchumi kataika misingi sahihi.Mungu ameahidi kukupa baraka nyingi sana kama uko tayari kusikiliza katika maagizo akuagizayo kila siku
(Kumb 28:1-13)
(3) MASHAKA NA KUTOKUAMINI JUU YA VITU UVIOMBAVYO KWA MUNGU WAKO
Watu wengi wanaomba sana kwa mda mrefu ili waweze kufanikiwa ili kutokana na mashaka na kutokuamini juu ya kila wakiombacho huchelewa kufikia mafanikio .Pamoja na kuomba mungu wako kulingana na imani yako ondoa mashaka na weka imani juu ya kile ukiombacho utakipa (Yakobo 1:6-8)
Ninakushukuru sana kwa kutenga mda wa kusoma maada hii .Mungu akubariki
Mada ijayo tutajifunza juu ya namna ya kujua kusudi ulilo itiwa kulitimiza
Ni mimi mpendwa wako Novath Kasiano
kwa masiliano zaidi nipigie kwa NO:0762 736 689/ 0753 485 656/0786 102 869
na barua pepe ni novathkasiano@gmail.com
No comments:
Post a Comment