KILA ALIYE
SIMAMA ALIANGUKA
Kuteleza
si kuanguka usemi huu ulisemwa na wahenga wakimanisha kuwa sio kila kujikwaa
kunasababisha kuanguka , unaweza ukateleza katika safari na usianguke ila
hauwezi kuanguka usipo teleza .Moja kati ya mambo ambayo ni kikwazo kikubwa kwa
watu wengi katika safari ya kuelekea mafanikio
ni kuanguka kwa mambo muhimu wanayokuwa wanategemea na inapokuwa
imetokea tayari mtu ambaye alikuwa
ameweka imani yake katika jambo hilo ambayo linaweza kuwa la kisiasa,
kiuchumi , kielimu, kiroho ,kimahusiano basi mtu huyo hupata anguko kuu linalo
anza moyoni . inawezekana unaposoma
makala hii tayari kuna mambo yameshakuangusha kiasi cha kuona kuwa hauwezi
kuinuka kabisa .Lakini leo napenda nikwambie kuwa kila aliye simama alianguka
.Ukipata mda wa kufatilia maisha yao utaona wazi kuwa hakika walianguka anguko
ambalo haikuwa rahisi kwao kuinuka tena ,tunaona mfano kwa aliyewahi kuwa raisi
wa Marekani Abraham Lincoln alianguka
zaidi ya mara arobainina saba(47) katika safari yake ya kuelekea mafanikio bila
kufanikiwa na katika anguko hilo aliaminikuwa siku moja atainuka na kufika
katika kilele cha mafanikio yake .Haikuwa rahisi kwa Lincolin kuinuka unaweza
ukajiuliza maswali kadha wa kadha nini kilimfanya Lincolin anguke mara safari
zote hizo , unaweza usipate majibu
sahihi ila nataka uone kuwa safari zote hizo ni matokeo ya kuwa kila alipo
anguka hakuamini kuwa ndiyo mwisho wa safari yake ,alicho kiamini nikuwa safari
yake itafika mwisho hadi pale atakapo fikia kila anachokiamini katika ndoto
zake.Hebu jiulize ni mara ngapi umeanguka katika safari yako ya mafanikio ?
Inawezekana umeanguka mara moja au zaidi ya mara moja jibu unalo wewe ,pamoja
na hayo inawezeka kana mpaka sasa tayari pamoja na kuanguka mara chache hizo
ulicho kwisha kuanguka na umeona kuwa tayari ni mwisho wako wa safari ya kuelekea
mafaniko.Anza leo kuweka imani hii kuwa kila haijalishi umekwisha kuanguka mara
ngapi katika Kilimo , Siasa , Mahusiano , Elimu, Biashara ,Unasanii wa nyimbo
za injiri au mziki wa kidunia, Uigizaji Michezo mbalimbali leo unaposoma makala
hii anza kuweka imani na kujiambia kuwa lazima
nifike mwisho wa kilele cha ndoto zangu.
Katika
kipindi hiki cha kuanguka katika safari ya kuelekea kwenye kilele cha mafanikio
kuna mambo muhimu lazima uyajua na kuyaishi ,leo napenda nikwambie mambo muhimu
mawili ya kujua na kuyaishi
Usimulaumu mtu yeyote
Lawama
ni moja ya jambo ambalo linakwamisha watu wengi sana katika kufika kilele cha
mafanikio yao kutokana na kuwa lawama huamsha hisia na maumivu makubwa mno
ambayo huongeza kiwango cha kukata tamaa.Pia lawama husiba nafasi ya kuziba
fursa ya kuona milango mingine ya ambayo
ingesaidia katika kutatua changamoto zinazofanya mtu aanguke tena lawama huondoa
ujasiri kwa mtu kuamini kuwa
kuanguka ni sehemu ya safari ya mafanikio ,lawama huondoa nguvu za mtu kuinuka
tena na kuendelea katika safari ya mafanikio ya kufikia ndoto zake.Hivyo
inawezekana tayari umeshaangushwa mara nyingi na watu
tena wakati mwingine waliokuangusha ni
Ndugu zako wa karibu ambao uliwaamini sana kuwa wangekusaidia
kufika
katika kilele cha safari ya mafanikio yako
lakini leo upo hivyo ulivyo kwa
sababu ya maumivu yaliyotokana na kulaumu watu uliowategemea ,haujachelewa
katika kipindi hiki usilaumu mtu yeyote badala yake pata mda mwingi wa
kutafakari sana mambo kadha wa kadha ambayo yamechangia kuangua katika jambo
ulilo litegemea kasha anza kuangalia na wengine mfano kama Abrahamu Lincolin
ambaye pamoja na kuanguka mara arobaini na sabu (47) bado akafanikiwa na kufikia katika ndoto yake ya kuwa raisi wa Marekani.Tabia ya
kulaumu kumewafanya watu wengi sana kufa na ndoto zao kwa sababu walipo
angushwa na watu wao wa karibu walianza
kuwalaumu na kupoteza tumaini kabisa kwa kuwaza kuwa haiwezekani tena kwa wao
kuinuka na kufika katika kilele cha mafanikio yao.
Amini ndoto yako
Kila
msafiri hupanga safari anayojua mwisho wake na atashangaa
sana asipofika mwisho wa safari yake anapajua anapotakiwa kwenda ila hatashangaa akifika
kwa kuwa alijua mwisho wa safari yao.Ndvyo ilivyo hata kwako wewew
unayesoma makala hii najua unayo ndoto
kubwa sana ambayo unaiamini kuwa siku
moja itatokea maishani mwako .Hijalishi
utaangushwa marangapi pengine na Ndugu zako au watu wako wa karibu wewe amnini
ndoto zako tu ,Abraham Lincolini
aliamini katika ndoto zake kuwa iposiku ataifikia ndiyo maana hata alipo
anguka zaidi ya mara 47 hakukata tama kwani angeshangaa kama asingekuwa raisi wa
taifa la marekani ila hakushangaa kwa kuwa
aliamini hivyo kuwa ndoto zake zingetimia
za kuwa raisi wa Marekani
Hitimisho
Usihesabu
juu ya mara ngapi umeangushwa bali fikiria ndoto zako zitatimia lini na
kadri utakavyo kuwa unafikiri mara kwa mara utajiongezea nafasi kubwa ya kuwa kufanikiwa kwa kuwa utaona mlango wa
kuku fanikisha katka ndoto zako.
No comments:
Post a Comment