Monday, 17 April 2017

MAMBO MKUU MATATU YANAYO CHELEWESHA MTU KUFANIKIWA KIUCHUMI

MAMBO  3 YANAYO CHELEWESHA MTU KUFANIKIWA KIUCHUMI


Mpendwa msomaji wangu leo napenda tujifunze juu ya mambo ambayo husababisha mtu kuchelewa kupata mafanikio ya kimaisha .
Kila binadamu aliyeumbwa na Mungu hutamani sana kuwa na mafaniko makubwa sana kiroho na kiuchumi .Katika jitihada za kufikia mafanikio hayo kila mtu huomba Mungu kulingana na imani yake ,lakini pamoja na jitihada hizo za kumuomba Mungu ili kufanikiwa kiuchumi yapo mambo makuu matatu yanayo chelewesha  mafanikio  yako  katika misingi sahihi

(1) KUTOKUJUA KUSUDI ULILOITIWA KUTIMIZA
Ni mpango wa mungu kumuumba mwanadamu ili alitimize kusudi lake ,lakini watu wengi sana wapo hapa duniani na hawajui kusudi lililo waleta kulitimiza hapa duniani hali ambayo inapelekea kuishi nje ya mpango wa mungu na kusababisha kuchelewa au kushindwa kabisa kupata kile wanacho sitahili kupata .Mungu anakujua hata kabla hajakuumba ,ila anachotaka kwako ni wewe kumuuliza  Mungu ujue kusudi alilokuitia ili uweze kulitimiza ,mfano Yeremia aliitwa kuwa nabii (Yermia 1:5) ukitambua kusudi la wewe kuwepo hapa duniani itakuwa rahisi kufikia mafanikio yako haraka

(2) KUTOKUSIKIA MAAGIZO YA MUNGU
Ni mpango wa mungu kwa mwanadamu kufanikiwa katika mambo yote  ila usipo  sikiliza maagizo ambayo mungu anakuagiza kufanya kila siku utachelewa kupata mafanikio kwani kila utakalo lifanya litakuwa nje ya mapango wa mungu .Mungu ame ahidi kukupa mambo mengi sana kama uko tayari kuyasikiliza  na kuyafanyia kazi maagizo akuamuruyo kuyafanya kila siku  utapata baraka nyingi sana ambazo  zitakupeleka katika mafanikio ya kimwili na kiuchumi kataika misingi sahihi.Mungu ameahidi kukupa baraka nyingi sana kama uko tayari kusikiliza katika maagizo akuagizayo kila siku
 (Kumb 28:1-13)

(3) MASHAKA NA KUTOKUAMINI  JUU  YA VITU  UVIOMBAVYO  KWA  MUNGU WAKO
Watu wengi wanaomba sana kwa mda mrefu ili waweze kufanikiwa ili kutokana na mashaka na kutokuamini juu ya kila wakiombacho huchelewa kufikia mafanikio .Pamoja na kuomba mungu wako kulingana na imani yako ondoa mashaka na weka imani juu ya kile ukiombacho  utakipa (Yakobo 1:6-8)

Ninakushukuru sana kwa kutenga mda wa kusoma maada hii .Mungu akubariki 
Mada ijayo tutajifunza juu ya namna ya kujua kusudi ulilo itiwa kulitimiza 

Ni mimi mpendwa wako Novath Kasiano
kwa masiliano zaidi nipigie  kwa NO:0762 736 689/ 0753 485 656/0786 102 869
na barua pepe ni novathkasiano@gmail.com


Friday, 7 April 2017

NGUVU YA NIDHAMU KATIKA KUFIKIA MAFANIKIO


M
                          NGUVU YA NIDHAMU KATIKA KUFIKIA MAFANIKIO

Nidhamu  ndiyo chanzo cha mafaniko yoyote ambyo mtu anatamani kuyafikia katika kutimiza ndoto zake .Mafanikio ya mtu hupimwa pindi anapokuwa ameanza kuishi ndoto zake ,mafanikio ambayo mtu anatafuta katika maisha ya kila siku  yamegawanyika katika makundi makuu matatu
1 Mafanikio kiuchumi.
Hili ni kundi mojawapolakupima mafaniko ya mtu , kwani ni ukweli usiopingika kuwa watu wengi hutamani sana kufanikiwa katika eneo la uchumi , kwa sababu mafanikio ya kiuchumi hufungua milango ya mafanikio mengine .Watu walio fanikiwa kiuchumi ndio pia wana nafasi ya kufikia mafanikio ya makundi mengine kwani mafanikio haya pia huleta pesa za kutosha ambazo ndo hizo zinazo leta jawabu la mambo yote( MUHUBIRI 10:19C)

2 Mafanikio kisiasa
Siasa ndiyo ambayo hutawala sana karibu mifumo yote ya kiutawala ambapo utawala uaotawala eneo flani ndio unao amua ana ya  mfumo wa kiuchumi wa eneo hilo .Wanasiasa wengi hutamani sana kufanikiwa katika eneo hili .Jambo moja muhimu ni kujua umuhimu wa kuwa na nidhamu ya kufatilia sana mambo ya husuyo siasa ili kupata taaifa nyingi na maarifa mengi ambayo yatakusaidia katika kufikia mafanikio kwenye eneo hili la siasa

Kama unataka ufanikiwe katika siasa anza leo kuweka nidhamu ya kufatilia sana maswala ya siasa ili kupata taarifa sahihi na maarifa mengi na utaona matokeo yatakayo kufikisha kwenye eneo hilisiasa ili kupata taaifa nyingi na maarifa mengi ambayo yatakusaidia katika kufikia mafanikio kwenye eneo hili la siasa


3 Mafanikio kiroho
Ni wazi kuwa kila mtu kutokana na imani yake katika dini yake anatamani  sana kukuwa kiimani (kiroho) na kukuwa huko kiimani(kiroho) hapo tunasema mtu huyu amefanikiwa
Licha ya mafanikio kugawanyika katika makundi makuu matatu nayo hutegemea mambo makuu matatu ambayo ni fedha , mda  na mipango mizuri
Leo napenda tuangalie nguvu ya nidhamu katika fedha , mda na mipango mizuri ili kufikia mafanikio  hayo

1 Nidhamu ya fedha
Fedha huleta jawabu la mabo yote (MUHUBIRI10:19C) ,ikiwa na maana kuwa fedha ndiyo nguzo ya kwanza  katika kuleta mafanikio makubwa kiuchumi , kisiasa na kiroho ikiwa tu utakuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha .Nidhamu nzuri ya fedha husaidia katika kutekekeza mipango mizuri  ili kufikia mafanikio . Mafanikio yako hayategemei wingi wala uchache wa fedha ulizo nazo bali hutegemea nidhamu katika matumizi ya kiasi cha fedha katika kuleta mafanikio .

2  Nidhamu katika matumizi ya mda
Waswahili husema mda ni mali lakini kama haujui dhana halisi ya usemi huu  utaona kama ni jambo la kawaida sana ,hata mimi kabla sijaelewa dhana ya msemo huu nilijua kuwa kitu cha msingi sana katika maisha ni kuweka nidhamu katika fedha na sio matumizi mazuri ya mda  ,lakini baada ya kujua thamani ya mda ningependa nukufahamishe nguvu ya nidhamu katika matumizi ya mda .Mungu ametupa mda wa masaa ishirini na nne (24) kila siku sawa na masaa elfu saba mia nane na sitini(7860) kwa mwaka mzima ila ni mda huohuo wapo watu matajili na watu masikini  sana ,hivi umewahi kujiuliza kwa nini watu wengi sio matajili au kwa nini watu wengi hawana mafanikio mkubwa  lakini kuna wachache wamefanikiwa sana wakati wote hao wana mda sawa kwa kila siku,siri kubwa ni kwenye nidhamu ya matumizi ya mda .Mafanikio yako yanategemea sana jinsi unavyo tumia mda wako vizuri katika kutimiza malengo yako.
 Anza leo kuwa na nidhamu katika matumizi ya mda katika mambo uliyopanga kuyafanya utaona matokeo

Nidhamu katika kutekeleza mipango yako
Kupanga ni kuchagua ,usemi huu umezoeleka sana masikioni mwa watu wengi sana ,lakini leo napenda nikwambie nguvu ya nidhamu katika kutekeleza mipango inavyoleta mafanikio haraka,katika mpango wowote katika kuleta mafanikio  kuna vitu vinaitwa vipaombele na maana ya vipaombele ni vitu vya msingi katika mpango wowote ambapo mafanikio ya lengo lolote hutegemea kukamilika au utekelezaji mzuri wa hivyo vipaumbele .ni wazi kuwa kila mtu ana mipango mbalimbali ya kutekeleza ili kufika mafanikio anayotaka na katika mipango hiyo kuna mikakati mbalimbali ya kutekeleza ili kufikia malengo hayo ,kitu cha muhimu kujua ili uweze kufanikiwa katika kufikia malengo yako ni kuweka nidhamu katika kutekeleza vipaumbele vitakavyo fanikisha mpango wako ,kwa maneno mingine ni kusema usikubali kutekeleza kipaumbele hata kimoja kwani kushindwa kukamilika kwa kipaumbele kimoja husababisha kushindwa kwa kukamilika mpango mzima ambao ndio ungekupelekea kufikia malengo yako . kinachotofautisha kati ya waliofanikiwa na amabao hawajafanikiwa ni nidhamu katika kutekeleza vipaumbele vya mpango wa kufikia malengo
Anza leo kuhakikisha unaweka nidhamu katika kuteleza vipaombele vya mpango uliojiwekea utaona matokeo mazuri sana katika kufikia malengo yako

Hitimisho 
Watu wote duniani walio fikia malengo yao walikuwa na nidhamu katika matumizi ya mda,fedha na mipango hata wewe haujachelewa anza leo kuwa na nidhamu katika matumizi ya mda ,fedha na mipango nakuhakikishia kuwa utafikia malengo yako