Wednesday, 15 August 2018

KILA ALIYE SIMAMA ALIANGUKA



                              
                         KILA ALIYE SIMAMA ALIANGUKA
Kuteleza si kuanguka usemi huu ulisemwa na wahenga wakimanisha kuwa sio kila kujikwaa kunasababisha kuanguka , unaweza ukateleza katika safari na usianguke ila hauwezi kuanguka usipo teleza .Moja kati ya mambo ambayo ni kikwazo kikubwa kwa watu wengi katika safari ya kuelekea mafanikio  ni kuanguka  kwa mambo muhimu  wanayokuwa wanategemea  na inapokuwa  imetokea tayari mtu ambaye alikuwa  ameweka imani yake katika jambo hilo ambayo linaweza kuwa la kisiasa, kiuchumi , kielimu, kiroho ,kimahusiano basi mtu huyo hupata anguko kuu linalo anza moyoni . inawezekana  unaposoma makala hii tayari kuna mambo yameshakuangusha kiasi cha kuona kuwa hauwezi kuinuka kabisa .Lakini leo napenda nikwambie kuwa kila aliye simama alianguka .Ukipata mda wa kufatilia maisha yao utaona wazi kuwa hakika walianguka anguko ambalo haikuwa rahisi kwao kuinuka tena ,tunaona mfano kwa aliyewahi kuwa raisi wa Marekani Abraham  Lincoln alianguka zaidi ya mara arobainina saba(47) katika safari yake ya kuelekea mafanikio bila kufanikiwa na katika anguko hilo aliaminikuwa siku moja atainuka na kufika katika kilele cha mafanikio yake .Haikuwa rahisi kwa Lincolin kuinuka unaweza ukajiuliza maswali kadha wa kadha nini kilimfanya Lincolin anguke mara safari zote  hizo , unaweza usipate majibu sahihi ila nataka uone kuwa safari zote hizo ni matokeo ya kuwa kila alipo anguka hakuamini kuwa ndiyo mwisho wa safari yake ,alicho kiamini nikuwa safari yake itafika mwisho hadi pale atakapo fikia kila anachokiamini katika ndoto zake.Hebu jiulize ni mara ngapi umeanguka katika safari yako ya mafanikio ? Inawezekana umeanguka mara moja au zaidi ya mara moja jibu unalo wewe ,pamoja na hayo inawezeka kana mpaka sasa tayari pamoja na kuanguka mara chache hizo ulicho kwisha kuanguka na umeona kuwa tayari ni mwisho wako wa safari ya kuelekea mafaniko.Anza leo kuweka imani hii kuwa kila haijalishi umekwisha kuanguka mara ngapi katika Kilimo , Siasa , Mahusiano , Elimu, Biashara ,Unasanii wa nyimbo za injiri au mziki wa kidunia, Uigizaji Michezo mbalimbali leo unaposoma makala hii anza kuweka imani na kujiambia kuwa    lazima nifike mwisho wa kilele cha ndoto zangu.
Katika kipindi hiki cha kuanguka katika safari ya kuelekea kwenye kilele cha mafanikio kuna mambo muhimu lazima uyajua na kuyaishi ,leo napenda nikwambie mambo muhimu mawili ya kujua na kuyaishi
Usimulaumu mtu yeyote
Lawama ni moja ya jambo ambalo linakwamisha watu wengi sana katika kufika kilele cha mafanikio yao kutokana na kuwa lawama huamsha hisia na maumivu makubwa mno ambayo huongeza kiwango cha kukata tamaa.Pia lawama husiba nafasi ya kuziba fursa ya kuona milango mingine ya  ambayo ingesaidia katika kutatua changamoto zinazofanya mtu aanguke tena lawama  huondoa  ujasiri kwa mtu kuamini  kuwa kuanguka ni sehemu ya safari ya mafanikio ,lawama huondoa nguvu za mtu kuinuka tena na kuendelea katika safari ya mafanikio ya kufikia ndoto zake.Hivyo inawezekana  tayari  umeshaangushwa mara nyingi  na watu  tena wakati mwingine waliokuangusha ni  Ndugu zako wa karibu ambao uliwaamini sana kuwa wangekusaidia

kufika katika kilele cha safari ya mafanikio yako  lakini leo upo hivyo ulivyo  kwa sababu ya maumivu yaliyotokana na kulaumu watu uliowategemea ,haujachelewa katika kipindi hiki usilaumu mtu yeyote badala yake pata mda mwingi wa kutafakari sana mambo kadha wa kadha ambayo yamechangia kuangua katika jambo ulilo litegemea kasha anza kuangalia na wengine mfano kama Abrahamu Lincolin ambaye pamoja na kuanguka mara arobaini na sabu (47) bado akafanikiwa  na kufikia katika ndoto  yake ya kuwa raisi wa Marekani.Tabia ya kulaumu kumewafanya watu wengi sana kufa na ndoto zao kwa sababu walipo angushwa na watu wao wa  karibu walianza kuwalaumu na kupoteza tumaini kabisa kwa kuwaza kuwa haiwezekani tena kwa wao kuinuka na kufika katika kilele cha mafanikio yao.
Amini ndoto yako
Kila msafiri hupanga safari anayojua mwisho wake  na atashangaa  sana asipofika mwisho wa safari yake anapajua anapotakiwa kwenda  ila hatashangaa  akifika  kwa kuwa alijua mwisho wa safari yao.Ndvyo ilivyo hata kwako wewew unayesoma makala hii  najua unayo ndoto kubwa sana ambayo unaiamini  kuwa siku moja  itatokea maishani mwako .Hijalishi utaangushwa marangapi pengine na Ndugu zako au watu wako wa karibu wewe amnini ndoto zako tu ,Abraham Lincolini  aliamini katika ndoto zake kuwa iposiku ataifikia ndiyo maana hata alipo anguka zaidi ya mara 47 hakukata tama  kwani angeshangaa kama asingekuwa raisi wa taifa la marekani  ila hakushangaa  kwa kuwa  aliamini hivyo kuwa  ndoto zake zingetimia za kuwa raisi wa Marekani
Hitimisho
Usihesabu juu ya mara ngapi  umeangushwa bali  fikiria ndoto zako zitatimia  lini  na  kadri  utakavyo kuwa unafikiri mara kwa mara  utajiongezea nafasi kubwa ya   kuwa kufanikiwa kwa kuwa utaona mlango wa kuku fanikisha katka ndoto zako.